Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada zaidi wa dharura wahitajika kwa wakimbizi wa ndani Iraq huku msimu wa Baridi ukiingia

Mkimbizi kutoka Iraq(Picha ya UNHCR)

Msaada zaidi wa dharura wahitajika kwa wakimbizi wa ndani Iraq huku msimu wa Baridi ukiingia

Serikali ya jimbo la Kurdistan na  Umoja wa Mataifa wametathmini mafanikio yaliyopatikana katika miezi ya hivi karibuni ili kukabiliana na mahitaji ya watu waliofurushwa makwao.

Umoja na Mataifa na serikali ya Kurdistan wametambua mahitaji ya haraka ya nyongeza ya dola millioni  152.2 ya  kugharamia mahitaji ya kimsingi kwa ajili ya raia karibu milioni moja wa Iraq.

Waziri wa Mpango wa serikali ya Kurdistan, Dr Ali Sindi amesema pamoja na changamoto, maendeleo mengi katika utoaji wa chakula, malazi, na afya yamefikiwa akiongeza kuwa lakini wanahitaji kufanya zaidi ili kupunguza mateso kwa wakimbizi.

Aidha, Sindi ametolea kipaumbele masuala ya kuwalinda watu kutokana na msimu wa baridi kali, chakula na shughuli ya kina ya usajili wa wakimbizi wa ndani.

Kulingana na Wizara ya mpango wa Kikurdi na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM, karibu nusu ya kila Iraq milioni 2.1 wamekimbia makwao.