Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali yaombwa kuridhia Mkataba kuhusu biashara ya silaha

Mlinda amani nchini DRC akikagua baadhi ya silaha zilizonyakuliwa huko Beni Kivuv Kasakazini.(Picha ya UM/Martine Perret)

Serikali yaombwa kuridhia Mkataba kuhusu biashara ya silaha

Serikali kote duniani zimetolewa wito wa kuridhia Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Biashara ya Silaha, ATT ambao utaanza kufanya kazi hapo kesho.

Ombi hilo limetolewa na kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa huru wa haki za binadamu ambao pia wametoa wito kuwekwa kikomo kwa biashara ya silaha.

Kufikia sasa ni nchi 60 tu ndizo zimeridhia  mkataba huo kati ya nchi 130 ambazo zimetia saini.

ATT ni mkataba wa kwanza wa kisheria wa kimataifa ambayo inazuia nchi kuuza silaha nje ya mpaka wake wakati wanajua silaha hizo zitatumika kwa ajili ya mauaji ya kimbari, uhalifu dhidi ya ubinadamu au uhalifu wa kivita.

Wataalam wanasema dunia haihitaji tu kusimamisha mauzo ya silaha bali pia faida zinazotokana na uzalishaji wa silaha zote.