Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pande kinzani Libya kukutana kwa mazungumzo

UN Photo/Rick Bajornas)
Picha:

Pande kinzani Libya kukutana kwa mazungumzo

Baraza la usalama leo limekuwa na mjadala kuhusu hali ya usalama nchini Libya ambapo Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, UNSMIL Bernardino León ameliambia baraza hilo kuwa kuna dalili za kufikiwa kwa amani kwa kuzingatia kuwa pande kinzani zitakuatana kufanya mazungumzo.

Bwana León amesema kuwa pande hizo zitakutana mano mwezi January mwaka 2015.

Wakati huo huo, wanachama wa Baraza la Usalama wameelzea wasiwasi wao kuhusu kuendelea kuzorota kwa hali ya Usalama nchini humo na mapigano yanayoendelea.

Halikadhalika, wanachama walielezea hofu yao kuhusiana na kuendelea kuingizwa kwa silaha haramu nchini Libya licha ya kuwepo kwa vikazwo.

Aidha, Baraza hilo lilisihi pande zote katika mzozo huo kusitisha mapigano maramoja na badala yake kushiriki katika mazungumzo ya amani.