Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti ya UNOSAT yaonyesha Uharibifu wa eneo ya Utamaduni Syria na kutoa wito wa ulinzi

Picha:UNESCO

Ripoti ya UNOSAT yaonyesha Uharibifu wa eneo ya Utamaduni Syria na kutoa wito wa ulinzi

Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Mafunzo na Utafiti, UNITAR, kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO leo imetoa ripoti muhimu inayobaini kwa kina uharibifu mkubwa wa maeneo ya urithi ya utamaduni nchini Syria.

Utafiti huo umefanywa na wataalamu wa urithi wa utamaduni Syria na wachambuzi wa picha za Satelite wa UNOSAT ambao walichambua maeneo 18 mapya  na kuonyesha kuwa maeneo 290 yameathiriwa na mapigano yanayoendelea.

Maneja wa UNOSAT, Einar Bjorgo amesema wakati huu wametoa ripoti hii ya kina ili kutoa tahadhari kwa watu wanaochukua hatua na umma kuhusu kuzorota kwa maeneo mengi ya utajiri wa urithi wa asili nchini Syria.

Mshirika hayo yametoa wito kwa jumuiya kimataifa kuunga mkono juhudi za UNESCO katika kutoa  ulinzi wa maeneo hayo.