Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO na washirika wa toa wito wa kimataifa kuhusu ugonjwa mpya wa ndizi.

UN Photo/Logan Abassi
Picha:

FAO na washirika wa toa wito wa kimataifa kuhusu ugonjwa mpya wa ndizi.

Shirika la Chakula na Kilimo duniani, FAO limesema juhudi za kimataifa zinahitajika ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa aina ya kuvu unaoshambulia ndizi ambao hufahamika kwa kitaalamu Fusarium ugonjwa ambao hudhoofisha ndizi , na hivyo kutishia ustawi wa kiuchumi na usalama wa chakula katika nchi zinazoendelea.

FAO imesema wanasayansi wa mimea wamekuwa wakionya kwa miaka kadhaa kuwa aina ya ndizi maarufu duniani ya Cavendish inakabiliwa na aina mpya ya Kuvu ambayo inasababisha kudhoofika na hatimaye kufa kwa ndizi.

Kwa maantiki hiyo, FAO na kundi la wataalamu wa kimataifa wamekubaliana mfumo wa kimataifa kuhusu ugonjwa huo ambao utahusu nyanja kuu tatu ya utekelezaji.

Mosi, kuzuia kuzuka kwa ugonjwa huo katika siku za usoni, pili kusimamia matukio ya sasa ya ugonjwa huo na tatu kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na uratibu kati ya taasisi, watafiti, serikali na wazalishaji wa ndizi.