Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yatoa wito wa msaada wa Kibinadamu kwa Peuhl CAR

Bouba Mairama akizungukwa na watoto, baadhi yao wakimbizi kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambaye anawalea nyumbani kwake katika Gbiti, Cameroon. Picha: UNHCR

UNHCR yatoa wito wa msaada wa Kibinadamu kwa Peuhl CAR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi, UNHCR limeelezea wasiwasi wake kuhusu hatma ya jamii ya zaidi ya watu 400 wanaoaminika kuwa waumini wa dini ya Kiislamu nchini Jamhuri ay Afrika ya Kati CAR ambao UNHCR imesema hali zao zimezorota. Taariofa zaidi na Amina Hassan.

(TAARIFA YA AMINA)

Akizungumza mjini Geneva msemaji wa UNHCR Adrian Edwards amesema jamii hiyo ijulikanayo kwa jina la Peuhl, kwa miezi kadhaa sasa imenaswa katika mji wa Yaloke ulioko karibu kilomita 200 Kaskazini maghrabi mwa mji Mkuu Bangui nchini CAR.

Kwa Mujibu wa Bw Edwards miongoni mwa watu hao, watu wazima na watoto wanakabiliwa na utapiamlo uliokithiri, asilimia 30 ya wakikumbwa na Malaria huku sita miongoni mwao wamethibitika kuuguwa kifua kikuu.

(SAUTI EDWARDS)

“licha ya kuwepo kwa vikosi vya kimataifa vya kulinda amani , kundi la watu walioko Yaloke bado wanakabiliwa na vitisho vya kila mara, matusi na uchokozi , na uporaji unaofanywa na wanamgambo wa Balaka. Msaada wa haraka wa kibinadamu unahitajika pamoja na msaada katika kuwahamisha watu hao hadi maeneo salama ndani ya CAR au nchi jirani”.

Edwards ameongezea kuwa tangu kuwasili mjini Yaloke mwezi Aprili watu 42 wamefariki huku wengine wakidhoofika kila uchao.