Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano ya mara kwa mara yanasababisha maafa na watu kukimbia Libya:Ripoti

Baraza la haki za binadamu kikao cha 18, mjini Geneva, Uswizi.(Picha ya UM/Jean-Marc Ferré)

Mapigano ya mara kwa mara yanasababisha maafa na watu kukimbia Libya:Ripoti

Mapigano ya hivi majuzi kati ya vikundi vilivyojihami magharibi,  mashariki na kusini mwa Libya yamesabibisha mamia ya raia kuuwawa huku wengine kukimbia makwao na kudhoofisha hali ya walio katika maeneo ya mizozo, hii ni kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu iliotolewa Jumanne leo mjini Geneva, taarifa kamili na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Ripoti hiyo iliyochapishwa kwa pamoja na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, UNSMIL na Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR imebainisha utekaji nyara wa raia, kuzingirwa kwa maeneo ya raia, mateso na ripti za kuwawa na uharibifu wa mali na ukiukaji wa haki za kimataifa kote nchini. Ravina Shamdasani ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu Geneva

“Makundi ya raia wametekwa na pande zote za mzozo sababu kuu ikiwa ni ukabila, familia au uhusiano wa kidini, kama wafungwa wa kubadilishana na waliotekwa katika pande kinzani. UNSMIL imepokea madai ya kuteswa na ukatili ambayo ni ukatili dhidi ya mateka, unaozua maswali na wasiwasi kwa ajili ya uhasama wa kisiasa na ukatili unaoshuhudiwa.

Ripoti imetaja wanaharakati wa haki za binadamu, waandishi wa habari na watu wenye ushawishi kwa umma kama walengwa na vikosi vilivyojihami huku wengi wakiripotiwa kutekwa, kutishiwa na nyumba zao kuporwa na kuchomwa.

Hivyo Kamisha Mkuu wa haki za binadamu Zeid Ra’ad Al Hussein ameonya pande mbili katika mzozo kwamba wana maswali ya kujibu kisheria na hata  kwenye mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai, ICC inayofanya uchunguzi nchini Libya.