Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama la jadili kuzorota kwa haki za Binadamu Korea Kaskazini

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu, Ivan Šimonovic.(Picha ya UM/video capture)

Baraza la Usalama la jadili kuzorota kwa haki za Binadamu Korea Kaskazini

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo alasiri limejadili kuhusu hali ya haki za Binadamu katika Jamhuri ya Kiemokrasia ya Korea Kaskazini, DPRKAkihutubia Baraza hilo Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu, Ivan Šimonoviæ amesema ni nadra sana kwa tuhuma nzito kama hizi kuwasilishwa  mbele ya Baraza la Usalama.

Kuhusu hali ya utawala wa nchi hiyo, Šimonovic amesema ripoti ya Baraza la Haki za Binadamu imeonyesha nchi hiyo iko chini ya utawala wa kiimla ambayo inatekeleza ukatili na unyama sawa na kunyima wananchi wake  haki ya uhuru wa mawazo, dhamira na dini, kama vile haki ya uhuru wa maoni, ya kujieleza.

(SAUTI Šimonoviæ )

Kwa mujibu wa uchunguzi wa Tume ya Baraza la Haki za Binadamu, uhalifu unaofanywa nchini Korea Kaskazini umeenena na kukithiri na kwamba ni sera ya makusudi inayoongozwa kutoka ngazi ya juu Serikalini. Na wakati mwingi matukio hayo yanaweza kuwa uhalifu dhidi ya ubinadamu”.

Hata  hivyo amesema tangu kuchapishwa kwa ripoti ya tume ya Uchunguzi wa Baraza la Haki za Binadamu, mamlaka ya DPRK imeonyesha ishara mpya ya ushirikiano na mifumo wa kimataifa ya haki za binadamu.