Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pakistan na Jordan waombwa kusitisha adhabu ya Kifo

UN Photos/ Paulo Filgueiras
Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, Zeid Ra’ad Al Hussein@

Pakistan na Jordan waombwa kusitisha adhabu ya Kifo

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, Zeid Ra'ad Al Hussein  ameelezea majuto yake kuhusu kuanza kwa adhabu ya kifo nchini Pakistan na Jordan wakati jumuiya ya kimataifa inazidi kuondokana na matumizi ya adhabu ya kifo.

Kmishina Zeid ameshutumu hatua ya hivi karibuni ya kurejeshwa kwa adhabu ya kifo katika nchi mbili, akisisitiza hakuna mahakama popote isiyokuwa na dosari.

Bw Zeid amesema ni bahati mbaya kwamba nchi ya Pakistan na Jordan zimmerudisha hukumu ya kifo na kwa hiyo kupunguza mda wa adhabu ya kifo ambayo walipendekeza mwaka wa 2008 na 2006.

Halikadhalika, Zeid amesema hatu hiyo ya Pakistan na Jordan ni yakukatisha tamaa kutokana na kwamba wiki iliyopita, mataifa 117 walipiga kura katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ya kusitishwa kwa matumizi ya adhabu ya kifo kimataifa.

Frej Fenniche, ni mkuu wa idara ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini katika ofisi ya Haki za Binadamu..

(SUATI ya Frej )

“Kuhusu Pakistan, mauaji hayo yametokea baada tu ya mauaji ya wiki iliyopita dhidi ya shule ya watoto. Ni ilikuwa ni kutisha watu labda. Sisi tunapinga adhabu ya kifo, ni kitendo cha kinyama , na pia utafiti umeonyesha kwamba adhabu ya kifo haiwezi kuzuia wauaji kutekeleza mauaji yao. Hata katika mifumo ya kisheria iliyoendelea sana, bado kuna uwezekano wa kukosea. Na adhabu ya kifo, ikitekelezwa, haiwezi kurekebishwa”