Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muongo mmoja baada ya tsunami Asia itayari kukabiliana na majanga

Picha: FAO

Muongo mmoja baada ya tsunami Asia itayari kukabiliana na majanga

Shirika la Chakula na Kilimo, FAO limesema miaka kumi baada ya janga baya la asili  kuwahi kutokea  Kusini na Kusini Mashariki mwa Asia,  mataifa katika ukanda huo yamejianda vyema kukabiliana na majanga kama tetemeko la chini ya bahari ya Tsunami lakini ikiongeza kuwa bado kuna nafasi ya kuboresha jinsi ya  kukabiliana na hali hiyo.Taarifa kamili  na Joseph Msami.

(Taarifa ya Msami)

Wakati wa janga hilo la Tsunami watu zaidi ya 200,000 walipoteza maisha yao huku maisha ya watu wengine milioni 1.4 yakisambaratika baada ya Tsunami kuharibu mashamba , mabwawa ya samaki, boti, zana za uvuvi na mifugo ambayo mfumo mzima wa uzalishaji wa chakula unategemea.

Mkurugenzi Msaidizi wa FAO na mwakilishi wa kanda ya Asia na Pasifiki, Hiroyuki Konuma amesema muongo mmoja baadaye, wakati wa kuadhimisha kumkumbu ya janga la Tsunami shirika la FAO linatathmini mafunzo yanayoweza kupatikana kuhusu kukabiliana na uharibifu wa  kilimo, usalama wa chakula na lishe yanayosababishwa na tukio kama hili la mabadiliko ya hali ya hewa.

Aidha, Bw Konuma amesema jumuiya ya kimataifa inapaswa kujifunza  na kuongeza kuwa kuna mengine ya kufanywa ili kuzuia na kupunguza maafa.