UNHCR yakomboa wakimbizi wa Syria walioko Iraq.

22 Disemba 2014

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi, UNHCR linawasaadia mamia ya wanafunzi wakimbizi wa  Iraq walioko nchini Syria kupata elimu na hivyo kubadilisha mustakbali wao japo hali ya mapigano imevuruga mfumo wa elimu nchini humo. Taarifa kamili na Amina Hassan.

(TAARIFA YA AMINA)

Mmoja wa walionufaika na mpango wa UNCHR ni binti aliyatajwa kwa jina moja Fatima ambaye licha ya ukosefu wa umeme amesom kwa bidii kila siku na kwa hiyo kufanya vyema katika mtihani wake wa shule ya sekondari.

Kwa udhamini wa UNHCR sasa Fatima atajiunga na Chuo Kikuu cha Damascus ili kusomea udaktari.

Azma yake ya baada ya kuhitimu ni kuwasaidia wairaqi wenzake kuwa na maisha bora.

Binti huyo amesema bila ya  msaada wa UNHCR, asingeweza  kwenda chuo kikuu.

Mpango huo wa elimu huu kwa wanafunzi wakimbizi wanaoishi  Syria  ulipozinduliwa mwaka 1999.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud