Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mshikamano na wajibu wa pamoja ni msingi wa SDG:Ban

Nembo ya siku ya mshikamano duniani.

Mshikamano na wajibu wa pamoja ni msingi wa SDG:Ban

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya mshikamano, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema siku hii imekuja wakati muafaka ambado mataifa yanaendelea kushikamana kuandaa ajenda ya maendeleo endelevu, SDG baada ya ukomo wa malengo ya milenia mwakani.

Amesema mshikamano unaodhihirishwa ni dalili kuwa pande zote iwe Umoja wa Mataifa, wawakilishi wa serikali, mashirika ya kiraia na watu binafsi wameguswa na lengo fursa hii muhimu.

Ban amesema ajenda mpya itazingatia watu na sayari ya dunia ikijikita kwenye haki za binadamu na mshikamano wa dunia wenye azma ya kuondoa watu kutoka lindi la umaskini, magonjwa na njaa.

Amesema msingi wake ni mshikamano na hivyo amesihi jamii ya kimataifa wakati huu wa kuandaa ajenda hiyo ya maendeleo endelevu, izingatia maadili ya msingi ambayo ni mshikamano na uwajibikaji wa pamoja.