Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yalaani mauaji Beni nchini DRC na kutoa wito ya misaada ya kuwafikia walioathiriwa.

Eneo la Eringeti, Beni, iliovunjika baada ya kupigwa risasi baada ya mashambulizi.(Picha/MONUSCO/Abel Kavanagh)

UNHCR yalaani mauaji Beni nchini DRC na kutoa wito ya misaada ya kuwafikia walioathiriwa.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi , UNHCR  limeelezea wasiwasi wake kuhusiana na mauaji na ukiukaji mengine ya haki za binadamu dhidi ya raia katika eneo la Beni Kaskazini mwa Mkoa wa Kivu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Taarifa zaidi na Abdullahi Boru.

(Taarifa ya Abdullahi)

Mashambulizi kadha katika miezi mitatu ya hivi karibuni yamesababisha kuenea kwa hofu na watu kufurushwa makwao.  Kwa maantiki hiyo, UNHCR imesihi kuwepo kwa nafasi ya kuwafikishia watu walio katika shida misaada ya kibinadamu.

Kwa mujibu wa UNHCR, kuna taarifa za kuaminika kwamba angalau watu 256, ikiwa ni pamoja na watoto, wameuawa kwa kutumia panga na shoka katika mashambulizi yaliyo tekelezwa kuanzia mwezi wa Oktoba. Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR

(SAUTI  EDWRADS)

 "Tunahitaji kuwezeshwa kuingia  maeneo hayo kwa usalama ili kutoa huduma za kibinadamu kwa wakazi hawa wanaotaabika. Mpaka sasa, imekuwa ni changamoto kubwa sana kwa wahudumu wa kibinadamu  kuwafikia wakazi wa  Beni na maeneo ya karibu yaliyoathiriwa na ghasia kwani jeshi la DRC linadhibiti mienendo kwenye maeneo hayo."

Halikadhalika, UNHCR imetoa wito kwa serikali ya DRC kulinda raia walioko Beni na maeneo ya jirani sawia na kuruhusu mashirika ya kibinadamu katika maeneo yaliyoathirika.