Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ombi jipya la usaidizi wa kibinadamu kwa Syria kulenga pia maendeleo

Wakimbizi wanawake wa Syria.Picha ya UNHCR/N. Daoud

Ombi jipya la usaidizi wa kibinadamu kwa Syria kulenga pia maendeleo

Wakati mapigano nchini Syria  yakiingia mwaka wa tano, Umoja wa Mataifa na wadau wake leo huko Berlin, Ujerumani wamezindua ombi jipya la usaidizi wa kibinadamu na kimaendeleo kwa zaidi ya raia Milioni 18 wa Syria.

Ombi hilo la zaidi ya dola Bilioni 8.4 lililowasilishwa kwa wahisani, linajumuisha usaidizi kwa wasyria Milioni 12 walio wakimbizi wa ndani nchini mwao na mamilioni wengine waliotapakaa nchi jirani.

Kwa mara ya kwanza ombi hilo linajumuisha misaada inayoweza kuchochea maendeleo kama anavyofafanua Sima Bahous Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa nchi za kiarabu.

(Sauti ya Sima)

“Hii imetokea kwa sababu ya uelewa wa jumuiya ya kimataifa na wahisani binafsi kwamba mgogoro wa Syria kwa mwaka wa kwanza na wa pili ulikuwa wa kijamii lakini kwetu sisi mgogoro unapoingia mwaka wa tano umekuwa wa kibinadamu na kimaendeleona tishio kubwa kwa amani na usalama katika kanda nzima, na kwamba kumekuwa na makubaliano mapana kuwa tunahitaji mbinu mpya katika kukabilia nao.”