Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazungumzo humaliza uhasama, yasema IPU ikigusia Cuba-Marekani

Nembo ya IPU

Mazungumzo humaliza uhasama, yasema IPU ikigusia Cuba-Marekani

Umoja wa mabunge duniani, IPU umekaribisha uamuzi wa Marekani na Cuba kuanza kuimarisha uhusiano  kati yao kufuatia mazungumzo kati yao yaliyoratibiwa na pande mbali mbali kwa miezi 18. Ripoti ya Grace Kaneiya inafafanua zaidi.

(Taarifa ya Grace)

Uamuzi huo, umekuja baada ya makubaliano ya kubadilishana wafungwa na hatua za kulegeza masharti ya usafiri, vibali dhidi wafanya biashara na wanadiplomasia, ambapo IPU imesema ni mwamko mpya baada ya miaka 50 ya uhasama wa kisiasa na kiuchumi kati ya mataifa hayo mawili jirani.

Rais wa IPU Saber Chowdhury amesema uhusiano mzuri kati ya majirani ni muhimu kwa amani ya eneo na usalama na hatua hii ni muhimu.

Ameongeza kwamba uamuzi huu wa kutafuta suluhu la uhasama wa miaka mingi ulikuwa umesubiriwa kwa muda mrefu na unahitajika.

Hatua hiyo ya Cuba na Marekani inahimiza moja ya kiungo muhimu cha IPU ambacho ni mazungumzo kama njia muhimu ya kutatua mizozo nz kuhakikisha suluhu za kudumu.