Sera za mazingira zainua matumizi ya vibanzi kwa ajili ya nishati:FAO

18 Disemba 2014

Uzalishaji wa bidhaa zote zitokanazo na mbao uliongezeka mwaka 2013 ikiwa ni mwaka wa nne mfululizo na hiyo ni kwa mujibu wa takwimu mpya zilizochapishwa leo na shirika la chakula na kilimo duniani, FAO. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

FAO imesema wakati utengenezaji wa mbao zitumikazo kwenye samani, ujenzi na hata vibanzi vya mbao vitumikavyo kwenye nishati uliibuka baada ya mdororo wa uchumi wa mwaka 2008-2009, uzalishaji wa malighafi za mbao zitumikazo kutengeneza makaratasi ulidorora mwaka 2012-2013.

Chanzo cha mporomoko huo ni China ambaye ni mnunuzi mkubwa kupunguza uchapishaji kwenye makaratasi na badala yake mfumo wa elektroniki kutumika kusambaza taarifa.

FAO imesema uzalishaji wa vibanzi vya mbao kwa ajili ya nishati uliongezeka kutokana na sera za nishati mbadala hususan huko Ulaya ikieleza kuwa mwaka 2013 zaidi ya tani Milioni 13 ziliuzwa duniani kote.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud