Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutoka kilimo cha Coka hadi Cocoa kubadili maisha ya wakulima Colombia

Mbegu za Cocoa zinazotumika kutengeneza chokoleti. (Picha@FAO)

Kutoka kilimo cha Coka hadi Cocoa kubadili maisha ya wakulima Colombia

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na udhibiti wa uhalifu na madawa, UNODC kwa ushirikiano na serikali za Colombia na Austria inaendesha mradi wa kilimo mbadala kwa wakulima wadogo kutoka kilimo cha zao la Coca linalotumika kutengeneza madawa ya kulevya aina ya Cocaine hadi Cocoa inayotengeneza Chokoleti.

Mradi huo uitwao Montebravo unaratibiwa na kampuni ya Chokoleti ya Austria na utawezesha wakulima 1250 kuacha kilimo cha Coka na badala yake wapande Cocoa ambayo siyo tu ikubalike bali pia itawapatia kipato cha juu zaidi.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa UNODC Aldo Lale-Demox amesema thamani ya vyanzo mbadala vya mapato inategemea bidhaa ambazo zinauzwa ndani na nje ya nchi akitolea mfano zao hilo la Cocoa ambalo sasa litauzwa Austria.