Bado haki inahitaji kutimizwa Burundi:Mtaalam

16 Disemba 2014

Ahadi ya kweli na haki bado inahitaji kutimizwa nchini Burundi ikiwa ni miaka 14 baada ya makubaliano ya amani na upatanisho ya Arusha amesema mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya mpito Pablo de Greiff mwishoni mwa ziara yake nchini humo.Amesema Burundi inayoelekea katika uchguzi mkuu mwakani imefanikiwa katika viwango kadhaa vya utulivu ambavyo ameviita msingi wa maendeleo ya mustakabali lakini akaonya kuwa mafanikio hayo yaweza kutoweka kirahisi.

Amesema maendeleo siyo tu suala la maendeleo ya kiuchumi akisisitiza kuwa kuwa sheria na haki za binadamu ni kiini cha msingi wa maendeleo. Akifafanua Bwana Pablo de Greiff amesema ili maendeleo yawe endelevu lazima kushughulikia ukweli, haki, fidia na kutambua juhudi zilizochukuliwa na serikali.

Amesema Burundi imeshuhudia vipindi kadhaa na matukio ya uhalifu tangu uhuru mwaka 1962 ikiwamo uvunjaji mkuu wa haki za binadamu nyingi ambapo matukio mengi ni ya kikabila.

Mtaalamu huru huyo ameonya kuwa serikali isiahirishe suala la kuendelea na uchunguzi dhidi ya uhalifu wa siku za nyuma akisema kuwa kinga zilizopo zimekuwa kikwazo katika haki dhidi ya upatikanaji wa haki katika makosa ya jinai

Ripoti yake inatarajiwa kuwasilishwa mbele ya baraza ala haki za binadmau mnamo September 2015

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter