Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tamaduni za mazishi ni Changamoto katika kupambana na Ebola Guinea: UNICEF

Wahudumu wa afya katika moja ya harakati za kinga na tiba dhidi ya ugonjwa huo huko Afrika Magharibi. (Picha@WHO)

Tamaduni za mazishi ni Changamoto katika kupambana na Ebola Guinea: UNICEF

Shirika la Umoja wa mataifa la kuwahudumia watoto, UNICEF limesema kuwaeleza wanakijiji waliopoteza mama au watoto wao kuwa hawawezi kuwazika jamaa zao kwa misingi ya utamaduni ni changamoto kubwa ambayo ni lazima ishughulikiwe ili kutokomeza ugonjwa wa Ebola  nchini Guinea.

Akizungumza na mwandishi wa Radio ya Umoja wa Mataifa Daniel Johnston huko Geneva, Uswisi baada ya ziara yake ya wiki mbili nchini Guinea ambapo kirusi cha Ebola kiligundulika Disemba mwaka jana, msemaji wa UNICEF Christophe Boulierac amesema kujaribu kubadili mila na desturi hiyo katika kipindi muda mfupi ni changamoto, lakini inawezekana

(SAUTI Boulierac 26’’)

"Wanapomzika mwanamke kwa kawaida wanasuka nywele zake . Lakini sasa hili haliwezekani kwani tumewaomba wasiwaguse watu wao. Kukosa kusuka nywele za mama yako, dada yako, ni kiwewe kubwa. Sisi ni lazima tuelewe kuwa uhamasishaji wa jamii unaweza kuwa muhimu mno na wenye manufaa, na mwishoni mwa wa siku huleta matokeo.”

Boulierac amesema suala la mila linagusa utamaduni wa ndani ya jamii husika ambalo pia limefungana na kudorora kwa usalama nchini Guinea.