Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji wanataabika, tuchukue hatua: IOM

Picha: IOM

Wahamiaji wanataabika, tuchukue hatua: IOM

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limetaka hatua za dharura zichukuliwe ili kuokoka maisha ya wahamiaji na kukomesha wasafirishaji haramu unaokatisha tamaa maisha yao na kujipatia kiasi kikubwa cha fedha. Taarifa kamili na Joseph Msami.

(Taarifa ya Msami)

Katika ujumbe wake kuelekea siku ya kimataifa ya uahamiaji Disemba 18 Mkurugenzi Mkuu wa IOM William Lacy Swing amesema kuwa takwimu zinaonyesha kuwa wahamiaji wengi hufa katika safari za hatari kwa kuwa na tumaini la kupata maisha bora kwao na familia zao.

Wahamiaji 4,000 walipoteza maisha mwaka huu pekee wakiwa baharini, milimani au pembezoni mwa  majangwa idadi inayofanya mwaka 2014 kuweka rikodi ya kipekee huku ikiwa ni mara mbili ya idadi ya wahamiaji waliokufa mwaka jana.

Kiwango kikubwa zaidi kilikuwa katika bahari ya Mediterranean, ambapo zaidi ya watu 3,000 walizama huku wahamiaji 540 waikufa huko Bengal barani Asia na wengine zaidi ya 307 walikufa wakati wakijaribu kuvuka mpaka kati ya Marekani na Mexico.

Swingi amesema ni lazima kushughulikia vichochezi vya ukataji tamaa vinavyowasukuma wahamiaji kwenda nchi nyingine kinyume na sheria na kutaka ushirikiano madhubuti. Mkuu huyo wa IOM amesema katika mapambano hayo wanasisasa wajasiri katika kupambana na kuongezeka kwa ubauzi wanahitajika ili kufanikiwa.

IOM inasema kwamba uwepo wa mizozo duniani ikiwamo nchini Libya, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Sudan Kusini, Syria, Iraq, uwpo wa homa ya akali ya Ebola pamoja na mabadiliko ya tabia nchi ni sababu za uhamiaji haramu.