Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunasisitiza mazungumzo siyo mapigano: UNSMIL

Nembo ya UNSMIL

Tunasisitiza mazungumzo siyo mapigano: UNSMIL

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, UNSMIL umelaani kuongezeka kwa shughuli za kijeshi nchini humo na badala unataka kufanyike kwa mazungumzo ya kisiasa.

Taarifa ya UNSMIL imesema kuongezeka kwa shughuli za kijeshi ni jaribio la moja kwa moja la kudhoofisha juhudi za mazungumzo ya kisiasa, na wanaohusika na shughuli hizo wana lengo la kuvuruga hatua ya kufikia ufumbuzi.

Kuhusu suala la la mafuta, ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa umesema, mafuta ya Libya ni mali ya watu wa Libya na halipaswi kuingiliwa na kundi lolote.

Halikadhalika, UNSMIL imesema idadi kubwa ya wananchi wa Libya wanataka mazungumzo  na hakuna njia nyingine kwani hakuna mshindi katika mapigano ya kijeshi kwani matumizi ya nguvu hayatafanikiwa kufikia malengo ya kisiasa.