Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mbinu mpya za uchunguzi zitasaidia vita dhidi ya ebola:WHO

Picha: WHO/S. Saporito — in Sierra Leone.

Mbinu mpya za uchunguzi zitasaidia vita dhidi ya ebola:WHO

Wakati harakati za kukabiliana na ugonjwa wa ebola zikiendelea, ulimwengu umeelekeza macho kwa juhudi zinazochukuliwa kutafuta njia salama na hakika za uchunguzi na tiba dhidi ya ugonjwa huo ambao umetikisa maeneo Magharibi mwa Afrika.

Shirika la afya duniani WHO, katika harakati za kuhakikisha uendelezaji chanjo linashirikiana na wadau ambapo siku ya Jumatatu limekuwa na kongamano mjini Geneva Uswisi la wawakilishi wa kampuni mbali mbali zinazotafiti kuhusu mbinu za upimaji wakiwemo pia wawakilishi wa mamlaka za dawa kutoka mataifa ya Afrika magharibi ambayo yameathiriwa pakubwa na ebola.

Katika kongamano hilo na waandishi wa habari Francis Moussy anayesimamia kitengo cha utafiti cha ebola amesema ni muhimu kwa nchi zenye mlipuko kuwa na maabara lakini akagusia changamoto kama vile muda mrefu kupata majibu, maabara mara nyingi ziko mbali na wagonjwa na kuna mkwamo kwenye teknolojia inayotumika kwa sasa.

WHO kwa kushirikiana na wadau waliwasilisha pendekezo la teknolojia mpya ya kufanya uchunguzi wa ebola.

(Sauti ya Moussy)

“Mbinu hizi mpya za uchunguzi zitawezesha uchunguzi wa haraka wa ebola na pia kuwezesha kufunguliwa upya kwa vituo vya afya vilivyofungwa kwa hofu ya kusababisha maambukizi ya virusi vya ebola.”