Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matumaini kwa ufumbuzi wa mgogoro Mashariki ya Kati yarejeshwe: Serry

Mratibu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati, Robert Serry(Picha ya UM/Loey Felipe)

Matumaini kwa ufumbuzi wa mgogoro Mashariki ya Kati yarejeshwe: Serry

Mratibu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati, Robert Serry amesema matumaini ya ufumbuzi wa kudumu kuhusu mgogoro kati ya Israel na Wapalestina ni lazima yarejeshwe  kabla ya kuchelewa zaidi.

Bw. Serry amesema hayo alipohutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya ripoti yake ya hivi karibuni kuhusu hali katika Mashariki ya Kati na suala la Palestina.

Mwanadiplomasi huyo amesema, licha  ya uchovu mkubwa kuhusu shughuli za amani, Israel na Wapalestina bado wanataka kumalizwa kwa mgogoro.

Amesema jamii ya kimataifa haiwezi kujiengua kwenye hali ya Palestina akigusia uamuzi wa hivi karibuni wa baadhi ya mataifa ya Ulaya.

(Sauti ya Serry)

Katika muendelezo wa mwenendo huko Ulaya, bunge la Ufaransa, Hispania, na Ureno yamepitisha maazimio yasiyo na nguvu kisheria yanaoomba serikali zao kutambua taifa la Palestina . Haya ni maendeleo makubwa ambayo yanaoyesha kuongezeka kwa ukosefu uvumilivu katika kuendelea kukosekana kwa maendeleo ya kweli katika kufikia ufumbuzi wa mataifa mawili yaani Palestina na Israeli , na kwamba serikali zinakabiliwa na mashinikizo  ya umma ya kuendeleza kumalizwa kwa mzozo huo kabisa.”

Mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa aliongeza kuwa hatua hizo si mbadala wa mchakato wa amani ya kweli ambao unahitaji mazungumzo ya pande zote mbili.