Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shughuli za utalii ni moja ya mbinu za kukabiliana na umasikini

Mji mkuu wa Kilwa Kisiwani na Songo Mnara ni miongoni mwa miji ya biashara ya kale na mfano wa sehemu za utalii nchini Tanzania.(Picha (15/03/2009) © UNESCO / Ron Van Oers

Shughuli za utalii ni moja ya mbinu za kukabiliana na umasikini

Ikiwa zimebaki siku chache kabla ya kufikia malengo nane ya milenia yaliyotolewa na umoja wa matafia, huku lengo namba moja kati ya malengo hayo likiwa ni kutokomeza umasikini uliokithiri na njaa. Huku ikisadifu kwa kina katika Kupunguza asilimia 50 ya idadi ya watu masikini ambao kipato chao ni chini ya dola moja kwa siku.

Pamoja na Kupunguza kwa asilimia hamsini idadi ya watu wanaokumbwa na njaa.

Mohammed Hammie kutoka radio washirika Pangani FM iliyopo mkoani Tanga nchini Tanzania, anatazama lengo hilo namba moja katika muktadha wa kuitumia fursa ya utalii katika kukabiliana na umaskini.