Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNESCO alaani mauaji ya mwandishi wa Marekani

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, Irina Bokova.Picha/UM/Amanda Voisard

Mkuu wa UNESCO alaani mauaji ya mwandishi wa Marekani

Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UNESCO, Irina Bokova ameshutumu vikali mauaji ya mwandishi wa habari raia wa Marekani Luke Somers aliyeuawa nchini Yemen.

Mwandishi huyo aliuawa pamoja na mwalimu mmoja wa Afrika Kusini Pierre Korkie hapo Disemba 6.

Wote wawili walikuwa wakishikiliwa mateka kwa kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja na kundi lenye misimamo mikali. Waliuwawa wakati wa jaribio la kuwaokoa lilipogonga mwamba katika kijiji kilichopo kusini mwa Yemen.