Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Harakati za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi nchini Tanzania

Eneo la kikokwe, mjini Pangani, Tanzania(Picha ya UM/Idhaa ya kiswahili/R.Katuma)

Harakati za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi nchini Tanzania

Kuanzia Disemba mosi hadi disemba 12 kumefanyika mkutano wa 20 wa nchi wanachama kuhusu masuala ya mazingira, COP20 huko Lima, Peru. Mkutano huo ulikuwa sehemu ya majadiliano ya kuwezesha kufikiwa na mkataba wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi mwakani huko Paris, Ufaransa.Majadiliano haya yanafanyika wakati tayari nchi zimeshuhudia athari za mabadiliko za tabia nchi ikiwemo:mmomonyoko wa udongo, ongezeko la kiwango cha maji ya bahari na athari zinginezo ambazo zimeathiri maisha ya watu. Basi ungana na Joseph Msami katika ripoti ifuatayo.