Makubaliano ya kudhibiti uchafuzi wa hewa Ulaya yaleta matumaini

12 Disemba 2014

Huko barani Ulaya kumefikiwa makubaliano ya kuwezesha kupunguza utoaji wa gesi chafuzi zinazoweza kusababisha magonjwa hatari kwa binadamu ikiwemo moyo na mapafu.

Gesi hizo chafuzi ni pamoja na Amonia inayopatikana wakati wa shughuli za kilimo mathalani kwenye mbolea ya samadi na itengenezwayo viwandani.

Makubaliano yamefikiwa baada ya mazungmzo yaliyoratibiwa na tume ya Umoja wa Mataifa barani Ulaya, UNECE ambapo afisa wake Alisher Mamadzhanov anaeleza madhara ya gesi hizo.

(Sauti ya Alisher)

 “Zinasababisha chembechembe iitwayo PM2.5 ambayo ni hatari sana kwani inaweza kuingia kwenye mapafu. Chembechembe hizi zimetambuliwa na shirika la afya duniani WHO kuwa zinasababisha vifo vinavyoweza kuepukika. Na sasa hivi uchafuzi wa hewa kwa ujumla unaongoza kusababisha vifo Laki Sita kila mwaka kwenye ukanda wa Ulaya na vifo Milioni Saba kila mwaka duniani kote.”

Makubaliano hayo yamepatia nchi za Ulaya mambo matano ya kuzingatia kupunguza utoaji hewa chafuzi kwenye sekta ya kilimo ambayo inatajwa kusabaisha asilimia 84 ya gesiya Amonia iliyoingia hewani mwaka 2012 kwenye ukanda wa Ulaya.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter