Uelewa wa athari kwa mazingira uende sambamba na hatua sahihi:Ban

11 Disemba 2014

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-moon amesema joto duniani linazidi kuongezeka sambamba na uelewa wa watu kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi.

Bwana Ban amesema hayo wakati wa mkutano wa ngazi ya juu wa mawaziri kuhusu hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi huko Lima, Peru ikiwa ni sehemu ya mkutano wa COP20.

Amesema kinyume na hali ya awali, sasa kuna uelewa kwamba dunia nzima iko kwenye mwelekeo mmoja wa suala hilo na njia pekee ya kukabiliana na mabadiliko hayo ni kubadilisha hali sasa kuwa fursa.

Kuhusu mikakati ya kukabiliana na mabdailko ta tabianchi Ban amesema wakati ndio sasa, na kwamba hatua zikichelewa, gharama itakuwa kubwa zaidi.

(Sauti ya Ban)

Kizazi kijacho ni lazima kiweze kuishi kwa uendelevu kwenye sayari yetu; kimazingira, kijamii na kiuchumi. Ni lazima tupate njia sahihi za kuchagiza maendeleo.”

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud