Utunzaji milima ndiyo suluhisho la maendeleo yetu : UN

11 Disemba 2014

Umoja wa Mataifa umesema kuwa milima ambayo inachukua asilimia 27 ya dunia inamchango mkubwa wa kusuma mbele ajenda ya maendeleo endelevu.

Katika taarifa yake ya kuadhimisha siku ya milima duniani inayoadhimishwa kila mwaka Disemba 11, UN imetaja baadhi ya faida zitokanazo za milima ikiwamo kuwepo kwa maji safi, nishati na chakula.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “ Milima kwa Kilimo” ikiwa na lengo  la kuleta uelewa kwa wananchi kuhusiana na kilimo cha kwenye milima ambacho ndicho kinatija kubwa kwa maendeleo endelevu.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud