Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

‘Nchi zikishirikiana zinaweza kuokoa roho za wahamiaji wanaozama’

Picha:UNHCR/A. Rodriguez

‘Nchi zikishirikiana zinaweza kuokoa roho za wahamiaji wanaozama’

Mashirika ya kimataifa ikiwemo yale ya Umoja wa Mataifa yamesema kuwa iwapo dunia itashirikiana kwa pamoja kuna uwezekano mkubwa wa kupunguza vifo vinavyowapata wahamiaji wakati wakiwasafiri baharini.

Katika tamko lao la pamoja mashirika hayo ikiwemo lile la uhamiaji IOM na mengine ya Umoja wa Mataifa yameeleza kuwa suala la kupunguza vifo hivyo vinavyoendelea kutokea ni suala linalowezekana iwapo kutakuwepo na ushirikiano kati ya nchi na nchi.

Yamesema jambo linalopaswa kuzingatiwa sasa ni kuhakikisha kwamba nchi zinazopokea wahamiaji, nchi ambazo wahamiaji hao wanatoka pamoja na maeneo wanayopitia kuweka ushirikiano ambao utazingatia kuheshimiwa kwa haki za binadamu na kujali utu wa kila raia.

Tamko hilo limetolewa kufuatia mkutano wa pamoja ambao uliwakutanisha maofisa kutoka IOM, Ofisi ya Umoja wa Matifa inayohusika na kukabiliana na uhalifu na dawa za kulevya pamoja na Ofisi ya Umoja  wa Matifa ya Haki za Binadamu.