Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utawala bora ni msingi wa amani na ulinzi Sahel: Mjumbe

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye ukanda wa Sahel barani Afrika, Hiroute (picha ya UM//Devra Berkowitz)

Utawala bora ni msingi wa amani na ulinzi Sahel: Mjumbe

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limeelezwa kuwa mivutano na mizozo huko Burkina Faso, Mali, Libya na Jamhuri ya Afrika ya Kati inaendelea kutishia usalama kwenye Ukanda wa Sahel. Taarifa kamili na Amina Hassan.(Taarifa ya Amina)

Baraza lilipokea ripoti kutoka kwa Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye ukanda wa Sahel barani Afrika, Hiroute Guebre Sellasie ambaye amesema Ebola ni tishio jipya lakini harakati zote za kuleta amani hazitazaa matunda iwapo nchi zenyewe hazitaimarisha utawala bora akitolea mfano Mali.

(Sauti ya Sellasie-1)

"Pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika mazungumzo baina ya makundi ya Mali huko Algiers, hali ya usalama kaskazini imedororoa na kuongezeka kwa mashambulizi makali dhidi ya walinda amani na jamii mpakani na Niger."

Mjumbe huyo akazungumzia uhusiano kati ya wahamiaji wanaovuka ukanda wa Sahel kwenda Ulaya na usalama eneo hilo.

(Sauti ya Sellasie-2)

"Kwa bahati mbaya uhamiaji huu utaongezeka katika hali ya sasa ya ulinzi na kibinadamu na inaweza tu kusababisha kuongezeka kwa vifo na kusababisha wahamiaji waliokataa tamaa kujiunga na makundi yaliyojiami."