Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa wakaribisha mchango wa Saudia wa takriban dola milioni 100

UN Photo/Albert Gonzalez Farran
Nchini Sudan.

Umoja wa Mataifa wakaribisha mchango wa Saudia wa takriban dola milioni 100

Umoja wa Mataifa umekaribisha msaada wa dola milioni 104 kutoka kwa Saudi Arabia kwa ajili ya Shirika la mpango wa chakula duniani WFP

Msaada huo unajumuisha dola milioni 52 za kusaidia wakimbizi Milioni 1.7 wa Syria na dola milioni 42 za msaada wa chakula kwa wakimbizi walioko nchini Ethiopia wengi wakiwa wa kutoka Sudan Kusini na dola milioni 10 zitasaidia kutoa chakula kwa wakimbizi walioko nchini Kenya.

Mkuu wa WFP Ertharin Cousin amesema kwamba fedha hizo zitasaidia kutoa msaada maramoja kwa watu wanaokabiliwa na njaa na wasio na uhakika na mustakhabali wao.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa shukrani zake kwa mfalme Abdullah bin Abdulaziz Al-Saud wa Saudia kwa moyo wake wa kujitolea kuwasiadia walio na mahitaji bila kujali wanatoka dini gani, au vikundi gani au kabila.