Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zeid aonya kuhusu kupuuza wahamiaji

UN Photo/Paulo Filgueiras
Kaminshna Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Mwanamfalme Zeid Ra’ad Hussen. Picha:

Zeid aonya kuhusu kupuuza wahamiaji

Wakati duniani leo ikiadhimishwa siku ya haki za binadamu, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu Zeid Ra'ad Al Hussein amesema kuwa suala la hamiaji linasalia kuwa moja ya kikwazo kikubwa duniani  na kwamba serikali zinapojaribu kuchukua hatua za haraka kukabiliana nalo zinapaswa kuhakikisha kwamba zinazingatia kulinda na kuheshimu misingi iliyopo katika haki za binadamu.

Amesema kuwa mataifa tajiri hayapaswi kujigeuza mageti ya kuwabana wahamiaji na kuongeza kuwa duniani kote wahamiaji hao wanaangua kilio wakitaka kutendewa haki.