Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tutatekeleza majukumu kukidhi matarajio: Profesa Assad

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali Tanzania Profesa Mussa Assad (Kushoto) akihojiwa na Assumpta Massoi wa Radio ya Umoja wa Mataifa. (Picha:RedioyaUM)

Tutatekeleza majukumu kukidhi matarajio: Profesa Assad

Hivi karibuni Tanzania ambayo ni mjumbe wa bodi ya wakaguzi wa Umoja wa Mataifa imepata Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali naye ni Profesa Mussa Juma Assad. Uteuzi wake unafuatia kustaafu kwa mtangulizi wake Ludovick Uttouh. Mara baada ya uteuzi na kuapishwa, Profesa Assad alifika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, kushiriki mkutano wa bodi hiyo ya wakaguzi inayojumuisha pia Uingereza na India.Assumpta Massoi wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa alipata fursa ya kuzungumza na CAG ambaye amezungumzia masuala kadhaa ikiwemo sakata la ESCROW na matarajio yake kuhusu masuala ya ukaguzi. Hapa anaanza kwa kuelezea lengo la mkutano anaohudhuria.