Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNMISS yaharibu silaha zilizopokonywa wakimbizi wa ndani

Wakati wa kutafuta silaha katika makazi ya wakimbizi naUjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS.(Picha ya UM/JC McIlwaine)

UNMISS yaharibu silaha zilizopokonywa wakimbizi wa ndani

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS umeharibu silaha za moto 25 na mamia ya visu, mapanga, na silaha nyingine ndogo ndogo zilizopokonywa wakimbizi wa ndani wanaoishi katika eneo la hifadhi ya raia kwenye mji mkuu Juba.

Tukio hilo limefanyika hadharani kwenye uwanja wa Tomping, likishuhudiwa na wanadiplomasia,  waandishi wa habari ambapo wafanyakazi wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya mabomu walichukua bastola, bunduki aina ya AK-47 vyuma, na  silaha zingine na kuziweka ndani ya mashine iliyozichakata katika vipande vidogo ili zisitumike tena.

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu huko Sudan Kusini na mkuu wa UNMISS Ellen Margrethe Loej amesema hatua ya leo na zitakazofuatia zitarejesha hali ya kiraia kwenye vituo vinavyohifadhi wakimbizi.

Tukio lingine kama la leo litafanyika baadaye mwezi huu katika kambi za UNMISS Malakal, Nassir, Wau, Bentiu and Bor.