Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika na Asia ndio maeneo hatari kwa wabunge

Nembo ya IPU

Afrika na Asia ndio maeneo hatari kwa wabunge

Kwa mujibu wa takwimu za mwaka huu za Umoja wa mabunge duniani, IPU Bara la Afrika na Asia ni maeneo hatari zaidi kwa wabunge wanaotetea haki za msingi za kibinadamu na kutumia  uhuru wao wa kujieleza.Ripoti hiyo imetolewa wakati wa kuelekea Siku ya Haki za Binadamu 2014 tarehe 10 mwezi huu ambapo IPU imesisitiza hatari zinazowakabili wabunge katika nchi kadhaa, madhalani kifo, mateso, vitisho, kukamatwa na kuwekwa kizuizini kiholela, ukosefu wa haki dhamana, kesi, ukiukaji wa uhuru wa kujieleza na kusimamishwa nyadhifa zao kinyume cha sheria kupoteza mamlaka zao bungeni.

Martin Chungong ni KatibuMkuu wa IPU

(SAUTI CHUNGONG)

“Wabunge duniani kote wako hatarini, wanakabiliwa na hali hatarishi, na wakati mwingine  wanakabiliana na matokeo mabaya kwa kufanya kazi yao, kwa kulinda haki za msingi za binadamu kwa kutekeleza haki yao wenyewe ya uhuru wa kujieleza.”