Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNSOM alaani shambulio la kigaidi Baidoa, Somalia

UN Photo/Rick Bajornas)
Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu, Somalia Nicholas Kay(

UNSOM alaani shambulio la kigaidi Baidoa, Somalia

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Nicholas Kay amelaani shambulio la kigaidi mjini Baidoa linalohofiwa kusababisha vifo vya watu kumi na watano na kujeruhi wengine  kadhaa.

Balozi Kay amenukuliwa akisema kuwa mashambilio kama hilo la Ijumaa usiku dhidi ya watu wa Somalia yanadhihirisha tabia ya kutojali ubinadamu na kuongeza kuwa watekelezaji wa shambulio wafikishwe haraka katika vyombo vya sheria.

Mwakilishi huyo maalum amesema kuwa Umoja wa Mataifa na ujumbe muungano wa Afrika nchini Somalia AMISOM, wamesaidia mamlaka  katika uokozi wa majeruhi ambao wanahitaji mataibabu zaidi mjini Mogadishu.

Amesema kuwa Umoja wa Mataifa unaendelea kusaidia watu wa Somalia ambao wanafanya kazi kwa kutambua tumaini lao kwa ajili ya amani na utulivu kwa mustakabali wa nchi.Balozi Kay ametuma salamu za pole kwa familia na jamaa walioguswa kufutia shambulio hilo lililoathiri pia wanasiasa na waandishi wa habari.

Katika hatua nyingine  UNSOM imesema inatambua kuwa bunge la Somalia limepiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu wa nchi hiyo Abdiweli Sheikh Ahmed na hivyo kumtoa madarakani.

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amempongeza Bwana Ahmed kwa juhudi zake za ujenzi wa amani na kusema kuwa anatarajia  uundwaji wa amani wa serikali baada ya kuondoka kwake ili kuendelea na ujenzi wa amani ya nchi hiyo.