Wastani wa bei ya vyakula haikubadilika kwa miezi mitatu mfululizo
Shirika la chakula duniani FAO limetoa ripoti ya bei ya vyakula kwa mwezi Novemba inayoonyesha kwamba kwa wastani bei ya vyakula haijapanda wala kushuka kwa miezi mitatu mfululizo tangu mwezi Septemba.
Vipimo vya bei vinazingatia mabadiliko ya bei ya vyakula ya kimataifa ikiwemo bei ya nafaka, nyama, bidha zitokanazo na maziwa, mafuta na sukari.
Ripoti ya mwezi Novemba inaonyesha kwamba bei ya mafuta na nafaka iliongezeka kidogo, huku bei ya bidhaa zitokanazo na maziwa na sukari ikishuka kidogo.
Kufuatia kusuasua kwa bei ya vyakula katika miaka ya hivi karibuni, vipimo vya bei ni vya chini ikilinganishwa na ilivyokuwa miaka minne iliyopita.
Sababu za kushuka kwa bei ni pamoja na wasiwasi kufuatia mabadiliko ya hali ya hewa.
Nchini Brazil kwa mfano, mvua iliondoa shaka ya kiangazi ambayo ingeathiri uzalishaji kwenye nchi hiyo inayoongoza kwa kuuza sukari duniani.