Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maeneo ya urithi wa utamaduni Syria na Iraq yalindwe:UNESCO

Picha: UNESCO

Maeneo ya urithi wa utamaduni Syria na Iraq yalindwe:UNESCO

Wakati mzozo ukiendelea huko Iraq na Syrai, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO Irina Bokova ametaka maeneo ya urithi wa utamaduni kwenye nchi hizo yawekewe aina maalum ya kuyalinda.

Akifungua mkutano wa kimataifa kuhusu vitisho dhidi ya urithi wa tamaduni na utofauti huko Paris, Ufaransa, Bokova ametaka hatua hizo zianzie huko Syria kwenye mji wa Aleppo hususan msikiti wa Omeyyad ambalo ni eneo la kipekee mjini humo.

Amesema bado hawajachelewa kuchukua hatua hiyo huku akilaani vitendo vya mauaji ya watu wa makabila madogo, mashambulio dhidi ya maeneo ya urithi wa utamaduni na uporaji wa mali hizo.

Naye Mshauri maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu uzuiaji wa mauaji ya halaiki, Adama Dieng amesema kinachoshuhudiwa Aleppo ni dhana ya utokomezaji wa tamaduni.