Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nyoka waleta kizaazaa huko Sudan Kusini

Mafuriko Sudan Kusini. Picha: UN-Photo-Isaac-Bill

Nyoka waleta kizaazaa huko Sudan Kusini

Watu 13 wamefariki dunia na wengine 10 kuwa katika hali mbaya baada ya kung'atwa  nyoka kwenye Jimbo la Warrap, nchini Sudan Kusini. Ripoti ya Amina Hassan inafafanua zaidi.

(Ripoti ya Amina)

Kamishna wa eneo hilo Wol Anei Anei amesema uwepo wa nyoka hao unafuatia mafuriko makubwa yaliyosababisha nyoka kukimbilia maeneo makavu ambako nako watu wamesaka hifadhi.

Amesema maeneo yalioathirika zaidi na mafuriko ni Toch Kaskazini, Toch Mashariki, Toch Magharibi na jur-mananger ambako nako wakazi wanahaha kujikwamua kutokana na njaa kwani hata barabara hazipitiki na hawawezi kwenda hospitali kusaka tiba.

(Sauti ya Anei)

" Tunatoa wito kwa mashirika yanayohusika na afya kuingilia kati janga hili, kwa kutumia helikopta helikopta ili kupunguza madhara, watu wana njaa, wakazi wa maeneo haya wanateseka"