Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR kuanzisha programu ya riadha kwa wakimbizi Burundi

Mama Furaha akipika katika nyumba ya rafiki yyake Cady ambaye aliwakaribisha nyumbani mwake.© UNHCR/A.Nijimbere

UNHCR kuanzisha programu ya riadha kwa wakimbizi Burundi

Katika juhudi za kuvumbua vipaji na kuwajumuisha wakimbizi katika shughuli za kijamii ikiwamo michezo, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR nchini Burundi kwa kushirikiana na kamati ya michezo ya  Olympiki, IOC wanaratibu michezo ya riadha kwa wakimbizi nchini humo.

Katika mahojiano na idhaa hii Mwakilishi Mkazi wa UNHCR nchini Burundi Abel Mbilinyi amesema tayari mchakato huo umeanza kwa hatua ya majadiliano na makao makuu ya UNHCR Geneva Uswisi.

(SAUTI MBILINYI)

Bwana Mbilinyi amesema kuwa wanatarajia mtaalamu kutoka IOC  atawasili hivi karibuni na kuanza programu maalum ya michezo kwenye kambi za wakimbizi.

Burundi inahifadhi wakimbizi kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na Rwanda.