Mitandao ya kijamii inawezesha usafirishaji haramu: IOM
Udhibiti dhidi ya usafirishaji haramu ni mgumu kutokana na wasafirishaji hao kutumia mitandao ya kijamii katika kuratibu shughuli zao na hivyo ni suluhisho la pamoaj linahitajika.
Akiongea na waandishi wa habari mjini New York msemaji wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM Leonard Doyle, usafirishaji haramu unakuwa kwa kasi akitolea mfano kuwa mwaka huu pekee watu zaidi ya 3,000 wamesafirishwa kiharamu kupitia bahari ya Mediterranean . Hata hivyo ameshauri mbinu mbadala kwa kutumia mitandao hiyo ya kijamii
(SAUTI DOYLE)
IOM inaangalia uwezekano wa kutumia mitandao hii kupaza sauti za wale waliotumikishwa kuwashawishi watu wasithubu kusafirisha katika njia hizi hatarishi . Tumejaribu kukabiliana na hili kwa njia tofauti. Kampeni za elimu ni ngumu hasa kwa kuzingatia kuwa wengi wana malengo ya kuishi maisha bora mijini
Katika hatua nyingine Bwana Doyle, amesema kuwa migogoro huko mashariki ya kati hususani vuguvugu la vikundi vya kigaidi ISIL vinachangia uhamiaji kwa kiwango kikubwa.
Kwa mujibu wa IOM migogoro na mdororo wa kiuchumi ni miongoni mwa sababu ya uhamiaji haramu.