WFP kupeleka msaada zaidi wa chakula Sudan Kusini: UM
Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP linatarajia kupeleka zaidi ya tani 400 ikiwa ni ziada ya chakula cha msaada wa chakula kwa kutumia basi Sudani Kusini.
Akiongea na waandishi wa habari mjini New York msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephanie Dujarric amesema msaada huo utatoka jimbo la White Nile hadi Upper Nile nchini Sudani Kusini . Hii inafuatia shehena ya kwanza iliyotumwa mwezi Novemba .
Katika hatua nyingine nchini Sudan mashirika ya Umoja wa Mataifa yamesema yamefanikiwa kutoa chanjo ya polio kwa zaidi ya watoto 500 katika majimbo ya Kordofan Kusini na Magharibi ambayo yametawaliwa na mizozo.
Amesema hii ni mara ya kwanza tangu mwaka 2012 watoto katika eneo hili wamepatiwa chanjo.