Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COP20 iweke mustakhbali sawia wa mazingira: Muyungi

COP20 iweke mustakhbali sawia wa mazingira: Muyungi

Wakati mkutano wa 20 wa nchi wanachama kuhusu masuala ya mazingira, COP20 unaendelea huko Lima, Peru wawakilishi wa nchi mbali mbali wamekutana kushiriki katika majadiliano ya kuwezesha kufikiwa kwa mkataba wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi baadaye mwakani huko Paris, Ufaransa.

Miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo ni Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira kwenye ofisi ya Makamu wa Rais nchini Tanzania, Richard Muyungi ambaye katika mahojiano na Assumpta Massoi wa Idhaa hii anaelezea lengo la mkutano na mambo wanayoyatarajia kutoka kwa mkutano huo, ungana naye