Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tukomeshe aina zote za utumwa: Ban

Mtazamo wa Kisiwa cha Goree, Senegal, ambayo ilikuwa kituo kikubwa cha biashara ya utumwa kwenye pwani ya Afrika kutoka karne ya 15 hadi19 . Picha: UNESCO / Dominique Roger

Tukomeshe aina zote za utumwa: Ban

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kumbukizi ya wahanga wa utumwa na biashara ya utumwa kupitia bahari ya Atlantiki kauli mbiu ikiwa ni ushindi dhidi ya utumwa kuanzia Haiti na kwingineko, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezitolea wito serikali, asasi za kiraia na sekta binafsi kuungana kukomesha aina zote za utumwa ukiwamo ule wa utumikishwaji.

Katika ujumbe wake kwa siku hii adhimu Bwana B an pia ametaka kufanyika kila liwezekanalo katika kuwasaidia mamilioni ya wahanga wanaotumikishwa na hivyo kunyimwa haki zao za msingi na utu.

Katika mahojiano maalum na idhaa hii mhadhiri Mkuu wa Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Dk. Benson Bana amesema ni jambo la kusikitisha kukumbuka utumwa lakini la muhimu ni

(SAUTI DK BANA)

Kadhalika mchambuzi huyo wa masuala ya kimataifa akatoa ushauri

(SAUTI DK BANA)