Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muziki watumika kuelimisha jamii kuhusu ebola

Picha: UNMIL Photo/Emmanuel Tobey

Muziki watumika kuelimisha jamii kuhusu ebola

Harakati dhidi ya Ebola zimeendelea kuchukuliwa ili kudhibiti mlipuko kwenye nchi zilizokumbwa zaidi huko Afrika Magharibi ambazo ni Liberia, Guinea na Sierra Leone. Umoja wa Mataifa kupitia ujumbe wake maalum wa kushughulikia dharura ya ugonjwa huo, UNMEER umekuwa ukisaka usaidizi ikiwemo ujenzi wa vituo vya tiba halikadhalika kampeni za uhamasishaji. Miongoni mwa kampeni za hivi karibuni zaidi ni ile inayotekelezwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia, UNMIL kupitia wafanyakazi wake. Kufahamu kwa kina kuhusu kampeni hiyo ungana na Assumpta Massoi katika makala hii.