Nabarro atathmini hatua za kukabiliana na Ebola Guinea

28 Novemba 2014

Hatua zilizopigwa na mamlaka za Guinea kukabiliana na kirusi cha Ebola nchini humo zinafanyiwa tathmini na mjumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ebola, Dkt. David Nabarro.

Takriban watu 5700 wamefariki dunia kutokana na mlipuko wa Ebola Afrika Magharibi katika nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone.

Katika mahojiano na Simon Ruf, Dkt. Nabarro amesema alizuru Guinea kwanza mwezi Septemba wakati maambukizi yakiendelea kwa kasi mno kuliko uwezo wa kukidhibiti.  Amesema sasa hivi anatathmini hali ilivyo kufuatia juhudi za kukabiliana na Ebola, na pia atazingatia hasa njia za ushirikiano baina ya serikali, wadau na Umoja wa Mataifa katika kuendeleza juhudi za kuukomesha mlipuko wa Ebola.

“Nimekutana leo na mabalozi kutoka nchi zinazojihusisha katika kuisaida Guinea, na nimeweza kuona jinsi wanavyoendelea kutoa uungaji mkono thabiti, na kuona ishara nzuri kuhusu jinsi juhudi za kupambana na Ebola zinavyoendelea, lakini pia kama kila mtu, bado wako makini katika kutaka kusaidia katika vita hivi, hadi pale kisa cha mwisho kitakapotibiwa.”

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter