Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNRWA yatangaza hali ya dharura Gaza kufuatia mafuriko

Picha: Ahmad Awad/UNRWA Archives

UNRWA yatangaza hali ya dharura Gaza kufuatia mafuriko

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumiwa wakimbizi wa kipalestina, UNRWA , limetangaza dharura katika mji wa Gaza, kufuatia hali mbaya ya hewa na mafuriko makubwa katika kipindi cha saa 48.

Katika taarifa, UNRWA imesema hakuna majeruhi au majeraha, hata hivyo mamia ya wakazi katika maeneo ya mafuriko karibu na mji wa Sheikh Radwan, wameathiriwa kwani maji ya mvua yamesomba makazi yao.

Aidha, shule moja ya UNRWA na kituo kimoja cha UNRWA cha kupokea watu katika mji wa Gaza vimeathiriwa na kupanda kwa kiwango cha maji.

Kama shirika kubwa la Umoja wa mataifa katika Ukanda wa Gaza, UNRWA inatumia uwezo wake wa vifaa na usambazaji kutoa mafuta ya dharura kwa manispaa, maji, vifaa vya kujisafi na afya, kupitia mashirika kama UNICEF na WHO.