Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lalaani shambulio mjini Kabul

Kikao cha Baraza la Usalama.(Picha ya UM/Rick Bajornas)

Baraza la usalama lalaani shambulio mjini Kabul

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali shambulio la November 27 lililotekelezwa kwenye gari la ubalozi wa Uingereza mjini Kabul nchini Afghanistan.

Shambulio hilo limesababisha vifo vya watu kadhaa na majeruhi kwa raia .

Kundi la wanamgambo wa Taliban wametangaza kuhusika na shambulio hilo.