Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO kukabiliana tatizo la miili kuzidi uwezo wa Antibayotiki

Antibiotics. WHO/S. Volkov

WHO kukabiliana tatizo la miili kuzidi uwezo wa Antibayotiki

Shirika la Afya Duniani, WHO, limezindua mpango mahsusi wa kukabiliana na tatizo la dawa za kuongeza kinga mwilini, yaani antibayotiki, kutoweza tena kufanya kazi kutokana na miili kushinda uwezo wa dawa hizo..

Wakitangaza kuzinduliwa mpango huo, wataalam wa WHO wamesema kuwa tatizo hilo sasa linaathiri sehemu kubwa zaidi ya jamii kuliko ilivyodhaniwa awali.

Dkt. Charles Penn kutoka WHO amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva kwamba tatizo hilo linaweza kumuathiri mtu yeyote katika jamii, akiongeza kuwa idadi ya vifo vitokanavyo na mwili kuuzidi uwezo wa antibayotiki kila mwaka na 25,000 katika nchi za Ulaya, na idadi sawa na hiyo Marekani.

Dkt. Penn